Majeshi 480 wa Nigeria watorokea Cameroon

Majeshi 480 wa Nigeria watorokea Cameroon
Wanajeshi 480 wa Nigeria wametorokea maisha yao nchi jirani ya Cameroon kufuatia makabiliano makali dhidi ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram.
Msemaji wa jeshi la Cameroon Luteini Kanali Didier Badjek amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wamepokonywa silaha na sasa wamewekwa katika shule .
Mapigano hayo yanawadia saa chache tu baada ya wapiganaji hao wa Boko Haram kutoa kanda ya video ambayo walitangaza kuundwa kwa himaya ya Kiislamu kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wanajeshi hao walikuwa wakikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau alizungumza kwenye kanda ya video iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji wake kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Gwoza mapema mwezi huu.
Haijabainishwa iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii Muungano wa wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic State inayotawala sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq na Syria.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria Chris Olukolade alipinga tangazo hilo akisema kuwa ''hakuna hata nchi moja ya taifa hilo iliyotwaliwa na kuwa Nigeria ni moja. ''
Kiongozi wa Boko Haram Shekao ametangaza himya ya KIislamu Kaskazini mashariki mwa Nigeria
Maelfu ya watu wameuwawa kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu 2009, wakati Boko Haram ilipoanza uasi wake.
Gwoza, iliyokuwa na wakazi 265,000 katika sensa iliyopita, ndiyo mji mkubwa zaidi ulio chini ya utawala wa Boko Haram.
Imepeperusha bendera zake juu ya Kasri ya Emir wa Gwoza, kiongozi wa kiasili wa mji huo, wakazi wanasema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment