wakiwa katika mazungumuzo
mazungumuzo yakiendelea
Mhe. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Juu wa Hospitali ya Iran, akiwemo Mkurugenzi Mkuu Dk. Asghar Fashad.
Mhe. Omar Mjenga akiwa akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Dk. Asghar Fashad.
Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai, leo amekutana na
kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Iran ya Dubai, Dr.
Asghar Fashad. Katika mazungumzo, Mhe. Mjenga alimuomba Dr asghar
kuangalia uwezekano wa kuwa na makubaliano kati ya hospitali yake na
Ubalozi Mdogo kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa Watanzania kwa
gharama nafuu ukilinganisha na gharama zake za sasa.
Baada ya mazungumzo na mashauriano ya muda wa saa moja, Uongozi wa Juu
wa Hospitali, ulikubali ombi la Mhe. Mjenga la kupunguza gharama za
matibabu kwa Watanzania kwa asilimia 40 (40%). Mwanzo, Uongozi
ulipendekeza asilimia 20, ambayo Mhe. Mjenga aliwaeleza kuwa bado
ilikuwa ni punguzo dogo na bado ingekuwa ni mzigo mkubwa kwa Watanzania.
Hatmaye, ndio maafikiano hayo yakafikiwa ya asilimia 40.
Mpango wa huu utajumuisha Watanzania wote waishiyo UAE na wale wanaoishi
nje ya UAE ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi Tanzania. Hospital ya
Irani ni moja ya hospitali zenye huduma za hali ya juu kwa hapa Dubai na
UAE kwa ujumla.
Uongozi wa Hospitali umekubali kuanza kutoa Vitambulisho Maalum kwa
ajili ya Watanzania wote kuanzia Jumapili tarehe 1 Septemba. Mkataba wa
Makubaliano haya utatiwa saini Jumatatu tarehe 2 Septemba.
Aidha, Mhe. Mjenga, amemuomba Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hii,
kuangalia uwezekano wa kujenga Hospitali kubwa yenye hadhi kama hii,
nchini Tanzania. Kimsingi, Mkurugenzi Mkuu amekubali ombi hili, na
ameahidi kumuomba Rais wa Hospitali kufanya ziara nchini Tanzania mwezi
ujao ili kuona na uongozi husika na kuanza mazungumzo ya kuanzisha
Hospitali kama hiyo. Ameeleza kuwa Tanzania na Iran na nchi marafiki wa
siku nyingi, na hivyo Iran inafarijika sana kuwa karibu na Tanzania
kimahusiano.
0 maoni:
Post a Comment