Ebola:Hofu yaendelea kutanda A.Magharibi



Liberia ni baadhi ya nchi zilizoathirika sana kutokana na Ebola
Kuna hofu kwamba mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, katika kanda ya Afrika Magharibi, utaendelea kuwa mbaya zaidi hadi kanda hiyo itakapopata afueni kutokana na ugonjwa huo.
Hii ni kwa mujibu wa maafisa wakuu wa afya nchini Marekani.
Mkurugenzi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa , Tom Frieden,amesema kuwa ugonjwa huo unahitaji hatua zaidi ili kuweza kuudhibiti.
Mawaziri wa afya katika kanda hiyo wanatarajiwa kukutana nchini Ghana kujadili hali ya ugonjwa huo ambayo inaendelea kuleta wasiwasi.
Shirika la afya duniani linasema kuwa ugonjwa huo umewaua watu 1,427.
Shirika hilo linasema kuwa huu ndio mlipuko mkubwa wa ugonjwa huo kuwahi kushudiwa na umewaathiri watu 2,615.
Nigeria imefunga baadhi ya shule kutokana na hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola
Liberia ndio nchi iliyoathirika zaidi kutokana na homa hiyo, huku watu 624 wakiripotiwa kufariki na wengine 1,082 kuambukizwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Bwana Frieden, alikutana na Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf kujadili njia za kupmbana na ugonjwa huo.
''Visa vya maambukizi vinaongezeka.Ni jambo la kusikitisha, lakini hivi ndivyo hali ilivyo, na huenda ikawa mbaya zaidi katika siku zijazo,'' alisema Bwana Frieden.
Mlipuko wa Ebola kama huu haujawahi kushuhudiwa. Kadhalika licha ya idadi ya walioambukizwa kuwa kubwa, tunafahamu kuwa kuna watu wengi zaidi walioambaukizwa na visa hivyo vimeripotiwa, '' aliongeza kusema bwana Frieden.
Alielea kwamba kuna umuhimu wa hatua za dharura kuchukuliwa na kuwataka wananchi wa Liberia kushirikiana kupambana na ugonjwa huo na pia kuachana na mienendo ambayo imechochea kuenea ugonjwa huo.
Licha ya fununu kwamba virusi vya homa hiyo havienezwi kupitia hewani na maji maji ya mwilini, kama vile damu au jasho, kutoka kwa wale walioambukizwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment