Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Posted Alhamisi,Agosti28 2014 saa 11:12 AM
Muundo wa Bunge ni moja ya mambo yaliyosababisha mvutano kwenye kamati karibu zote 12, kiasi cha suala hilo kuundiwa kamati ya watu kumi ndani ya Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu.
Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amelazimika kuandika waraka kuhusu mapendekezo ya kitaalamu na kuyawasilisha mbele ya Kamati Namba 11 baada ya kuibuka malumbano makali kuhusu aina ya muundo wa Bunge unaotakiwa.
Gazeti hili liliona nakala ya mapendekezo hayo ambayo baadaye Othman alikiri kuwa ni yake.Mwansheria huyo ambaye msimamo wake ni mfumo wa Muungano wa Serikali tatu, amependekeza Bunge kuwa na sehemu mbili (bicameral).
Muundo wa Bunge ni moja ya mambo yaliyosababisha mvutano kwenye kamati karibu zote 12, kiasi cha suala hilo kuundiwa kamati ya watu kumi ndani ya Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu. Suala jingine ambalo lilizua utata ni idadi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Sehemu moja iwe na wajumbe kutoka Tanzania Bara pekee na ishughulikie mambo yasiyo ya Muungano kwa Tanzania Bara na sehemu ya pili iwe na idadi ndogo ya wabunge kwa idadi sawa kutoka pande mbili za Muungano na ishughulikie mambo ya Muungano pekee,” inasema sehemu ya waraka huo.
0 maoni:
Post a Comment