Rais Barack Obama wa Marekan
amesema mapigano yanayoendelea nchini Ukraine si matokeo ya kukua kwa
maasi nchini humo bali ni uchochezi wa Urusi.
Amesema waandamaji nchini Ukraine wamekuwa
wakifanya vitendo hivyo kutokana na uchochezi wa Urusi ambapo anadai
kuwa nchi hiyo inahusika katika kuwasaidia silaha na gharama za fedha
waasi hao.Hata hivyo Rais Obama hajatoa mrejesho wa moja kwa moja kwa kile ambacho NATO wamekiita umuhimu wa kuongeza majeshi ya Urusi nchini Ukraine.
Obama pia ameionya Urusi kwamba kwa kufanya hivyo itakuwa gharama kubwa kwao na pia yaweza kuwasababishia hasara.
0 maoni:
Post a Comment