Rubani wa kwanza wa kike nchini
Kenya sasa amepata mafanikio zaidi kwa kufuzu kuwa rubani wa kwanza
mwanamke barani Afrika kushika usukani wa ndege za kisasa aina ya Boeing
787 Dreamliner.
Imemchukuwa Rubani Irene Koki Mutungi kipindi
cha zaidi ya miaka ishirini kufanikiwa kuvunja pingamizi zote
zinazowazuia wanawake kuingia katika taaluma hiyo inayotawaliwa na
wanaume. Mwandishi wa BBC Denis Okari alifanikiwa kukutana naye baada ya kutua kutoka ndege hiyo ambayo ni ya nne katika msafara wa ndege mpya aina ya Dreamliner zinazomilikiwa na shirika la ndege la Kenya Airways.
Alianza kazi yake ya kuendesha ndege mwaka 1993.
Kazi yake ya kwanza hata hivyo ilikuwa aliposhika usakani wa ndege ya Fokker 50 kwenda Kisumu Magharibi mwa Kenya kama kazi ya kwanza ya kulipwa.
Alianza kupenda kuendesha ndege alipokuwa msichana mwenye umri wa miaka 17.
Alianza masomo yake katika chuo cha mafunzo ya uendeshaji ndege cha Oklahoma nchini Marekani.
Anasema angependa zaidi kuwasaidia wasichana wengine wa kiafrika na pia kuanzisha wakfu wake wa kuwasaidia watu masikini katika jamii.
0 maoni:
Post a Comment