Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi (katikati-meza
kuu) akiwa na wajumbe wa Kamati hiyo wakati walipokuwa wanawahoji waomba
hifadhi (hawapo pichani) katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo
Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi mbalimbali
ambapo wengi wao ni Wakongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanahojiwa
na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali ambazo
ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya Wakimbizi,
Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Inspekta Jererali
wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia
Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo.
Mwenyekiti
wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi
(watatu kushoto), Katibu wa Kamati hiyo, Philo Nombo
(watatu kulia) ambaye anamwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi
nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo baada
ya kuwahoji waomba hifadhi katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu,
iliyopo
Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi mbalimbali
ambapo wengi wao wanatoka nchini Kongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanaendelea
kuhojiwa na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali
ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya Wakimbizi,
Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Inspekta Jererali
wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia
Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
0 maoni:
Post a Comment