VAN GAAL HUWEZI KUPIKA CHAPATI KWA UNGA WA MUHOGO.

Tunashukuru aliye leta wazo la kila kata kuwa na shule ya sekondari.shule hizi kwa kiasi zimesaidia kufuta ujinga kwa walio wengi .Asilimia kubwa kwa wanao maliza shule za msingi wanapata nafasi za kuingia kidato cha kwanza tofauti na enzi zile za mwalimu,na mzee wa Ruksa ,heri nusu shali kuliko shali kamili,ingawa shule hizi zinawalakini lakini mchango wake ni mkubwa kwa jamii na unaonekana ,tofauti ya sasa na zamani inaonekana kupitia shule hizi wa awajaelimika ila wamepunguza shali kwa kufuta ujinga wengi wao angalau wanajua kujieleza kwa lugha ya chakula.pia wengi wanajua ukichanganya Hydrogen na oxygen unapata maji ukichukua sodium na chlorine unapata Chumvi na ukitaka kupata chumvi kwa pamoja ni lazima uchanganye Acid na Base.


hii ndo tunaita Chemistry(chemia)kwa ufupi chemia ni masomo ya Atomi na mkusanyo wa Atomi kuwa molyekuli,hata ndungu za ngu wajenzi wanajua hilo hili upate zege ni lazima uchanganye ingredients iliupate zege ni lazima uchanganye maji,kokoto mchanga na simenti kwa viwango maalumu.

Kocha Van Gaal wa Manchester United kama akukimbia somo la chemestry basi anataka kutoonyesha staili mpya ya kupika chapati kwa unga wa muhogo.Van Gaal amethubutu kutengeneza molyekuli ya 3-5-2 lakini amekosa Atomi usika za kutengeneza chemestry kwenye timu.watu wa mpira wana elewa kuwa eneo la kiungo ndio muhimu kuliko nafasi nyingine uwanjani kama unavyo jua tafsili ya kiswahili neno kiungo pia ndio hivyo hivyo tafsiri hiyo utumika katika soka,katika soka viungo ndio waunganishaji wa mawasiliano kati ya mabeki na washambuliaji timu nzuri ni hile yenye viungo imara.

                                                                   na
                                                       Anthony      fuzzu   
                                                        0765441559.      
      
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment