KATIBU wa CCM Mkoa wa Arusha,
Mary Chatanda, amekumbwa na fyagio katika uhamisho wa Makatibu wa Mikoa
uliofanywa na chama hicho.
Chatanda ambae alituhumiwa na
Umoja wa Vijana wa CCM wa mkoa wa Arusha kwa kuingilia mambo ya ndani ya
jumuiya hiyo, amehamishiwa mkoa wa Singida.
Zainab Shomari Katibu wa CCM
mkoa wa kusini Unguja, anakwenda likizo kwa miezi miwili na Shija Othman Shija,
amepelekwa mkoa wa Tanga kutoka kusini Pemba.
Mwangi Kundya, aliyekuwa Katibu
wa mkoa wa mjini Unguja amehamishiwa
Mbeya, Joyce Masunga amehamishiwa Pwani kutoka Mwanza, Alphonce
Kinamhala amehamishiwa Arusha kutoka Katavi na Jeneth Kayanda sasa anakuwa
Katibu wa mkoa wa Tabora kutoka Bukoba mjini.
Wengine waliohamishwa ni Gustav
Muba anaekwenda Geita kutoka Tanga, Sauda Mpambalyota anaekwenda Kusini Unguja
kutoka Pwani na Evelyne Mushi anaekwenda Katavi kutoka Kagera.
Aidha aliekuwa Katibu wa mkoa
wa Singida, Naomi Kapambala, amehamishiwa Kigoma, Idd Ame amehamishwa kutoka
Tabora kwenda Kagera, Mohamed Nyawenga amehamishiwa mjini Unguja kutoka Kigoma
na Adam Ngalawa amehamishiwa Mara kutoka Shinyanga.
Maganga Sengelema amehamishiwa
Shinyanga kutoka Mbeya, Marry Maziku, amehamishiwa makao makuu Dodoma kutoka
Geita na Benard Nduta amehamishiwa Mwanza kutoka makao makuu Dodoma.
Wakara wa uhamisho huo ulisainiwa na Katibu Mkuu
wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana.
0 maoni:
Post a Comment