Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar imesema haina Ubaguzi wa aina yoyote katika kugawa Miche ya
Mikarafuu badala yake inaangalia namna ambavyo Mkulima katayarisha
mashamba yake kwa ajili ya kupanda zao hilo.
Afisa kutoka Kitengo
Dhamana cha Utoaji wa Miche ya Mikarafuu Badru Kombo Mwenvura ameyasema
hayo wakati alipokuwa akijibu tuhuma zilizotolewa na Wakulima wa Karafuu
katika kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema si kweli kuwa
Miche hiyo hutolewa kwa misingi ya itikadi ya Vyama na kwamba Kitengo
husika cha kutoa Miche ya Mikarafuu huitoa kwa Mkulima yoyote
aliyekamilisha masharti.
“Kwa kweli lazima
tuweke wazi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijadhamiria
kuwabagua wananchi wake na hasa Wakulima wa Zao la Karafuu katika
kuwapatia Miche.
0 maoni:
Post a Comment