Mkurugenzi
wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila akisisitiza jambo kwa waandishi
wa habari.
Mkurugenzi
wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila akionesha barua za kuomba vibali
vya kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini.
Mkurugenzi
wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila (kushoto), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu maandamano ya
chama hicho yatakayoanza kesho nchini kote kupinga Bunge Maalumu la
Katiba linaloendelea Dodoma. Kulia ni Kada wa Chadema, Aron Mashuve na
Mwanasheria wa chama hicho, John Malya.
Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akimkaribisha Kigaila kuzungumza na wanahabari.
Mwanasheria wa Chadema, John Malya akifafanua baadhi ya vipengere vya sheria kuhusu ruhusa ya kufanya maandamano.
Mwanasheria wa Chadema, John Malya akiwa na kada wa chama hicho, Aron Mashuve.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesisitiza kuwa migomo na
maandamano yasiyokoma nchi nzima yapo palepale na kwamba yanaanza rasmi
kesho kwa kishindo kikubwa na hakuna mtu wa kuyazuia kwani ni haki yao
kikatiba.
Chadema
kimesema lengo la maandamano hayo ni kuishinikiza Serikali ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kitoe tamko la kusitishwa Bunge Maalum la Katiba
linaloendelea mjini Dodoma huku likifuja fedha za wananchi.
Kauli
hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Organizasheni na
Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaila wakati akizungumza na wanahabari
Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni.
"Maandamano
yaliyotangazwa na Freeman Mbowe si ya kwake ni maazimio ya Mkutano Mkuu
wa Chadema uliofanyika Septemba 14, mwaka huu.
"Tunasisitiza
kuwa maandamano na migomo isiyokoma nchi nzima yapo palepale, lengo
letu ni kuishinikiza Serikali isitishe Bunge la Katiba kwani mkutano
mkuu uliazimia jambo hilo baada ya kuona kuwa kinachofanyika Dodoma
hakitatupa Katiba Mpya, bali fedha za wananchi zinatafunwa bure"alisema.
Aidha,
alisema maandamano yao yapo kisheria ambapo katika Katiba ya nchi,
maandamano ni haki sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992
kifungu cha 11 kifungu kidogo cha 1 inaruhusu jambo hilo.
Kigaila
aliongeza kuwa sheria hiyo inataka waandamanaji kutoa taarifa ndani ya
saa 48 kabla ya na si kuomba kibali taratibu ambazo wao wameshazipitia.
"Natoa
mwito kwa Watanzania wote wakatae ufisadi unaofanywa na Bunge Maalumu
la Katiba. Kilichoko Dodoma ni kumaliza fedha ambazo zingetumika
kujengea nyumba za walimu au hata zahanati katika maeneo mbalimbali
nchini,"alisema .
Kigaila
alisisitiza kuwa wamepata barua kutoka Jeshi la Polisi kuwataka
kusitisha maandamano lakini hawatasitisha kwa sababu, sababu za katazo
hazina mashiko na hazijanukuu kifungu chochote cha sheria.
Alisema licha ya wao Chadema, maandamano yao hayo yamepata baraka kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Mkurugenzi
huyo wa organizasheni wa chama hicho alisema maandamano hayo
yanafanyika katika ngazi ya majimbo, wilaya na mkoa, ambapo kwa mkoa
yataanzia maeneo tofauti kuishia ofisi za mkuu wa mkoa husika na kwa
wilaya yatakwenda kwa mkuu wa wilaya husika.
Alisema
maandamano hayo kila mahali yataanza asubuhi, huku kwa mikoa mitatu ya
kanda ya Dar es Salaam yataanza keshokutwa Jumatano.
Kwa
upande wale Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya alisema sababu
nyingine iliyotolewa na polisi kuwa maandamano hayawezi kufanyika kwa
sababu kesi iliyofunguliwa Saedy Kubeinea ya kupinga Bunge hilo ipo
mahakamani kuwa haina mashiko kwa kuwa Chadema ni taasisi
inayojitegemea na inamaamuzi yake ya kichama.
0 maoni:
Post a Comment