MOSHI:
JAIZMELALEO
Dereva wa bodaboda ambaye
hakufahamika jina lake mara moja amenusurika kufa, katika ajali ya pikipiki
mapema leo asubuhi mjini Moshi mara baada ya kugongwa gari lisilofahamika na kutoweka
kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea majira ya
saa 4:30 asubuhi maeneo ya Idara ya Maji katika Manispaa ya Moshi likihusisha
magari mawili na pikipiki moja.
Mashuhuda wa tukio hilo
wamesema gari dogo aina ya taxi ambalo lilikuwa likitokea Majengo liliigonga
pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba vifaa vya ujenzi baada ya kuchelewa kuwasha taa
ya kuomba kuvuka barabara.
Waliongeza kusema baada ya
dereva wa bodaboda kuomba njia aliruhusiwa na ghafla alibamizwa kiupande upande
hali iliyosababisha dereva wa gari afunge breki mara moja na pikipiki kuburuzwa
upande mwingine ambako gari la abiria lililokuwa likifanya safari zake kati ya Sido
na KCMC (pichani) lilisimama ghafla na kunusuru maisha ya dereva huyo.
Maafisa wa Jeshi la Polisi mkoa Kilimanjaro walifika
eneo la tukio dakika chache baadaye.
Y
0 maoni:
Post a Comment