Raia wa Sierra Leone
wamesalia majumbani mwao kwa siku ya pili mfululizo wakati ambapo taifa
hilo linatekeleza agizo la kutotoka nje la masaa 72 ili kujaribu
kusitisha ueneaji wa ugonjwa wa Ebola.
Mwandishi wa BBC katika
mji mkuu wa Freetown anasema kuwa barabara nyingi za miji ambazo
zimekuwa zikijaa watu hazina watu kwa sasa.
Mwandishi wetu
anasema kuwa kituo cha oparesheni za dharura kilipokea zaidi ya simu 900
katika siku ya kwanza ya agizo hilo,kupitia kuwaripoti wagonjwa ama
kutaka miili ya wafu kuchukuliwa.
Amesema kuwa kuna vituo viwili pekee katika taifa hilo na kwamba kituo kimoja katika eneo la Kenema kimejaa wagonjwa.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment