Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro
Ltd. wadau na wananchi wakijipanga tayari kuanza kampeni ya wiki tatu
ya kusafisha maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji iliyozinduliwa rasmi
na Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi ikiwa ni awamu ya kwanza kwa
mwaka huu kabla ya kuelekea kwenye kata nyingine mbili zilimo ndani ya
manispaa ya Ilala wakishirikiana na wananchi.
Na Mwandishi wetu
WILAYA ya Ilala imeanzisha kampeni ya wiki tatu
ya usafi katika maeneo yaliyopo katikati ya Jijini la Dar es salaam
kwa lengo la kutoa elimu na kuyaweka maeneo hayo safi na salama.
Kampeni hiyo ilizinduliwa mwishoni mwa juma katika eneo la Kisutu na Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi .
Akizundua kampeni hiyo alisema bila suala la usafi kufanyiwa kazi, wageni wataona kwamba mambo katika Jiji la Dar e s salaam ni hovyo hasa ikizingatiwa kwamba kati ya jiji ndio sebule ya Jiji.
Kampeni
hiyo inayosimamiwa na kampuni yenye dhamana ya usafi katika eneo hilo
la kati ya Green Waste Pro Limited inashirikisha wananchi kwa lengo la
kuwafanya wawe washirika wa usafi kwa kujenga utamaduni wa kuchukia
uchafu.
Mkuu
huyo wa wilaya pamoja na kushukuru wananchi na wanafunzi wa shule ya
Kisutu waliofika katika kampeni aliwataka viongozi kujipanga
kuhakikisha kampeni hiyo inakuwa endelevu na yenye mafanikio.
Kampeni hiyo inafanyika katika kata ya Kivukoni, Kisutu na Mchafukoge.
Pamoja
na Mkuu huyo wa wilaya kusema kwamba kampeni hiyo ni chachu kwa kata za
pembezoni za kujali usafi amewataka wananchi kuwa washiriki kw
akuhakikisha hawatupi uchafu hovyo.
Naye
Naibu Meya na Diwani wa Kisutu Kheri Kessy alisema kazi ya usafi
inakabiliwa na changamoto kubwa hasa kutokana na kuvuja kwa chemba za
maji machafu na wananchi kutupa taka hovyo.
Alisema wananchi na hasa wapiti
njia kama wakijifunza kutupa uchafu maeneo wanayotakiwa watakuwa
wamesaidia sana kujenga utamaduni wa kuchukia uchafu na pia kufanya
maeneo yapendeze.
Alisema
wananchi wa kata yake ya Kisutu ni waelewa tangu kuanza kwa kampeni
hizo miaka miwili iliyopita lakini wapiti njia wamekuwa wakivuruga
utaratibu wa usafi.
Aliwataka
wakazi wa dare s salaam kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha hawatupi
taka hovyo na kuanza kuuchukia uchafu kutoka katika majumba yao hadi
wanakotembea.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony
Mark Shayo (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya
madiwani wa kata tatu zilizomo ndani ya manispaa ya Ilala na watendaji
wa halamshauri ya manispaa ya Ilala wakati wakimsubiri mgeni ramsi
kuzindua kampeni ya wiki tatu ya kusafisha maeneo yanayozinguka manispaa
hiyo wakianzia katikati ya jiji. Kushoto ni Meneja Msaidizi wa Kampuni
ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena.
Kampuni
inayoendesha kampeni hiyo ya Green Wate kupitia kwa meneja wao Abdallah
Mbena amesema kwamba kuna maendeleo makubwa katika kamepni za kuweka
Jiji safi na safari
hii wamewaalika wenzao kutoka Segerea na Upanga ili waone njia
wanazotumia kuweka maeneo yao yenye dhamana safi na ya kupendeza.
Mbena
alisema changamoto kubwa zinazokabili juhudi za kuweka maeneo safi ni
upungufu wa usimamizi katika sheria kwani wengi hawakubali kuzitii.
Alisema
kama wangelizitii kungelikuwa na usafi kila siku. Kwani wengine
wamekuwa wakifika katika majengo yao na kuyasafisha na kutupa uchafu
barabrani wakati wafagiaji wameshafanyakazi yao usiku.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni
ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro
Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (katikati) na Meneja Msaidizi wa Kampuni ya
Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena wakijadiliana jambo kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kampeni hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati) akizungumza na vyombo vya
habari na wananchi wa Kata ya Kisutu muda mfupi kabla ya kuzindua
kampeni ya chukia uchafu katika kata tatu za wilaya hiyo. Kata hizo ni
Kisutu, Mchafukoge na Kivukoni. Kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya
Ilala, Kheri Kessy na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi
iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw.
Anthony Mark Shayo.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Kheri Kessy akizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa rai
kwa wananchi wa kata hizo kuunga mkono kampeni hiyo yenye lengo la
kung'arisha vitongoji vya manispaa ya Ilala na wengine waige kutoka
kwao.
Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya wasichana ya sekondari Kisutu na wafanyakazi
wa Green Waste Pro ltd. waliojumuika na kampuni ya Green Waste Pro Ltd
kuunga mkono kampeni hiyo ya iliyopewa jina na Mkuu wa wilaya ya Ilala
ya "Chukia uchafu".
Mkuu
wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala
Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo kwenye picha ya pamoja na
watendaji wa manispaa ya Ilala na madiwani wa kata hizo tatu.
Baadhi ya madiwani na wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd. wakimwaga taka kwenye gari maalum la kampuni hiyo kwenye maeneo ya katikati ya jiji wakati wa kampeni hiyo iliyoanza mwishoni mwa juma.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya
Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (aliyebeba jiwe)
akishiriki zoezi hilo.
Zoezi
la usafi likiendelea ikiwemo kukusanya madumu ya maji pamoja na maboksi
ya wauza matunda na mboga mboga yanayozagaa maeneo ya Kata ya Kisutu
kama inavyoonekana pichani.
0 maoni:
Post a Comment