Hatukutoa taarifa kwa Syria, yasema Marekani

Afisa Mkuu wa Marekani amesema nchi hiyo haikutoa taarifa yoyote rasmi kwa utawala wa Syria juu ya  mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu mapema leo. Msemaji wa  Wizara ya  mambo ya nchi za nje  Bibi Jen Psaki alisema pia kwamba hawakushirikiana kwa njia yoyote na serikali ya Syria katika utekelezaji wa mashambulizi hayo.
Hata hivyo Psaki alisema utawala wa Syria uliarifiwa moja kwa moja kupitia Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power, aliyempa taarifa Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja huo. Awali Syria ilisema inaunga mkono hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Dola  la Kiislamu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment