Obama asema nchi yake haiko peke yake katika vita dhidi ya IS

Rais wa Marekani Barrack Obama amesema muungano wa nchi za kiarabu zilizoshiriki katika shambulizi la kwanza la Marekani katika mapambano dhidi ya wanamgambo walio na itikadi kali wa Dola la Kiislamu IS nchini Syria, umeonyesha kuwa Marekani haiko peke yake katika mapambano kwa wanamgambo hao. Obama pia ameonya kuwa operesheni dhidi ya kundi hilo huenda ikachukua muda, lakini atafanya kila liwezekanalo kuwashinda wanamgambo hao. Mashambulizi hayo ya angani yanayotekelezwa na Marekani na baadhi ya mataifa ya kiarabu yalianza siku ya jumatatu usiku yakilenga makao makuu ya wanamgambo wa IS Mashariki mwa Syria.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment