KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FUNUA MAGOKO (35) MKAZI WA ITUMBI ALIUAWA KWA
KUPIGWA FIMBO SEHEMU ZA KICHWANI NA WATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.
LUGANO GEORGE (33) NA 2. MOSSES MWACHILA (30) WOTE WAKAZI WA ITUMBI
WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEOMAJIRA YA SAA 00:30 HUKO KATIKA
KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO NI KULIPA KISASI KWANI
INADAIWA KUWA MAREHEMU NA WENZAKE WANA TUHUMIWA KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA
MAUAJI.
WATUHUMIWA WAMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO
MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 07 – 09 AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE MARA MOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE
NAMBA ZA USAJILI T.916 APD AINA YA SURF HILUX IKIENDESHWA NA DEREVA
AITWAYE KEFFA MAHENGE (29).
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.08.2014 MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI HUKO
MAENEO YA SOGEA – TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA,
MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI
LIPO KITUONI.
KATIKA TUKIO LA TATU:
DEREVA
ALIYEKUWA AKIENDESHA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.495 ALM AINA YA
NISSAN PICK UP ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BONIFACE MWASOBA AMEFARIKI
DUNIA BAADA YA GARI HILO KUACHA NJIA NA KUPINDUKA MAENEO YA NANENANE
DARAJANI JIJI NA MKOA WA MBEYA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:30 HUKO MAENEO YA
NANE NANE DARAJANI, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/IRINGA. AIDHA KATIKA AJALI HILO WILLY
BONIFACE MWASOBA (07) MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MKAPA ALIJERUHIWA NA
AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. GARI LIPO ENEO LA TUKIO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA DEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 maoni:
Post a Comment