Akiongea
na kipindi hiki afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten amesema kuwa
kikosi hicho kinataraji kutua jijini Mbeya ijumaa ya kesho kikiwa na
msafara wa watu 25 viongozi 5 na wachezaji 20.
Ten
ameongeza kuwa timu hiyo ianataraji kuwa kipimo kizuri kwa timu ya
Mbeya City kwani mmoja ya timu amabazo zimeonyesha uwezo mkubwa katika
ligi ya Uganda na kufanikiwa kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa
ligi kuu ya nchi hiyo.
Huu
utakuwa mchezo wa mwisho wa kujipama nguvu kwa Mbeya City kabla kuanza
mbilinge la ligi kuu ya soka Tanzania bara inayotaraji kuanza kutimua
vumbi September 20 kwenye viwanja mbalimbali.
Mbeya
city ambayo ilikamata nafasi ya tatu msimu uliopita kwenye ligi kuu ya
soka Tanzania bara inaendelea na mawindo yake chini ya kocha mkuu Juma
Mwambusi na msaidizi wake Suleiman Jabir
Afisa
habari wa Mbeya City Dismas Ten amewaomba wakazi wa Mbeya kujitokeza
kwa wingi katika mchezo huo jumapili kuishuhudia timu yao pendwa
ikionyesha kile ambacho imejipanga nacho kwa ajili ya ligi kuu ya soka
Tanzania bara msimu wa mwaka 2014/2015.
0 maoni:
Post a Comment