Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye maonyesho Katika Uwanja wa Taifa.Picha na Maktaba.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa mazoezini.
Kwa hisani ya Josephat Lukaza – Lukaza Blog.
Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo limetimiza Miaka 50 toka Kuanzishwa
kwake mnamo tarehe 1/09/1964. JWTZ ni moja ya Jeshi lililotajwa na
Mtandao mmoja hivi karibuni kuwa Ni Jeshi lenye weredi wa hali juu
Duniani kutokana na Operesheni ambazo limewahi kuzifanya na linalotumia
Silaha za Kisasa. Baadhi ya Operesheni zilizowahi kufanywa na Jeshi la
Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) ni Ile ya Kuwasambaratisha Waasi Wa M23
nchini Congo, Operesheni ya Comoro, Operesheni nyingine ni Ile ya
Kulinda Amani Sudan wakiwa wameungana na Majeshi Mengine Kutoka Umoja wa
Mataifa (UN)
Jeshi la
Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) limejipatia Umaarufu na sifa kutokana na
Kuwa na Askari wenye Nidhamu ya Hali ya Juu na Kuwachukulia Hatua kwa
Haraka Askari wake ambao wameonyesha utovu wa Nidhamu kwa Wananchi na
Jamii kwa Ujumla lakini Pia Sifa Hiyo Kubwa Imekuja Kutokana na uwezo
mkubwa wa Kivita na Kuweza Kuwasambaratisha Waasi wa Kikundi cha M23
nchini Congo.
Jukumu
kubwa la Kazi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni Kulinda Mipaka ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Wavamizi na Vile vile Kushiriki
katika kulinda Amani Katika Ngazi ya Kimataifa lakini Pia Pamoja na
Majukumu hayo vilevile Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa
Mstari wa Mbele katika Kujitoa kwenye shughuli za Kijamii kama Vile
Matibabu, Elimu nk na Wamekuwa Mstari wa Mbele katika Kusaidia Jamii
katika shughuli mbalimbali kama Vile za Uokoaji katika Maafa yanayotokea
Nchini.
Kwa
kifupi Sasa hivi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa jeshi la
Kisasa na wasomi ambao wanalisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo
yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa
katika shughuli nyingine za kijamii. Hongera ya Kutimiza Miaka 50 Tokea
Kuanzishwa
0 maoni:
Post a Comment