TAMASHA
kubwa la umataduni linalojulikana kama 'Handeni Kwetu' limepangwa
kufanyika Desemba 13 mwaka huu, katika Uwanja wa Azimio, wilayani
Handeni, mkoani Tanga.
Mratibu
Mkuu wa Tamasha la Handeni Kwetu, Kambi Mbwana, akizungumza jambo
katika tamasha la mwaka lililofanyika Desemba 14. Mwaka huu tamasha hilo
litafanyika Desemba 13, Siku ya Jumamosi, katika Uwanja wa Azimio,
wilayani Handeni, mkoani Tanga. Picha na Maktaba Yetu.
Wasanii
wa kundi la ngoma za asili la Mgambo JKT, wilayani Handeni, mkoani
Tanga, wakitoa burudani katika tamasha hilo mwaka jana. Mwaka huu
litafanyika Desemba 13, Siku ya Jumamosi, katika Uwanja wa Azimio,
wilayani Handeni, mkoani Tanga. Picha na Maktaba Yetu.
Mkuu
wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu (katikati), akifurahia katika
tamasha hilo mwaka jana lililofanyika Desemba 14. Mwaka huu litafanyika
Desemba 13, Siku ya Jumamosi, katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni,
mkoani Tanga. Kulia kwake ni Afisa Utawala wa wilaya ya Handeni, Upendo
Magashi. Picha na Maktaba Yetu.
Katika
tamasha hilo linalofanyika kwa mara pili, burudani mbalimbali za ngoma
za asili zinatarajiwa kuonekana jukwaani, ambapo pia vikundi kutoka nje
ya Handeni, mkoani Tanga navyo vitaalikwa kwa ajili ya kwenda kutoa
burudani wilayani humo.
Akizungumzia
hilo, jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana,
alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yanawekwa ili kuliweka katika
kilele cha ubora na kuchangia maendeleo ya sanaa na uchumi kwa ujumla.
Alisema
kuwa mwaka jana tamasha hilo lilianza kwa mafanikio makubwa, ambapo
wageni mbalimbali walifika wilayani humo, jambo lililochangia pia
kuitangaza Handeni na mkoa mzima wa Tanga.
“Mwaka
huu tumeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa tamasha letu
linaendelea kukua kwa kasi baada ya kuanzishwa kwa mafanikio makubwa
mwaka jana.“Naamini kuwa haya ni matunda ya kushirikiana kwa pamoja na
wadau wote, ikiwamo serikali kwa kupitia ofisi zote za wilaya ya
Handeni, hivyo watu wajiandae mambo mazuri na makubwa kutoka kwenye
tamasha hili,” alisema Mbwana.
Tamasha
la utamaduni la Handeni, linalojulikana kama Handeni Kwetu, ni miongoni
mwa matamasha yenye mchango mkubwa, ambapo kwa mwaka jana Shirika la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) ndio waliokuwa wadhamini wakuu na kufanikiwa kwa
kiasi kikubwa kuliweka katika mguso wa aina yake.
0 maoni:
Post a Comment