Somalia:Wakazi wahisi kuwa salama

Wakazi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wanahisi kuwa salama na wenye matumaini zaidi kuliko hali ilivyo kuwa mwaka mmoja uliopita.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya masomo ya sera, ambayo ilitathmini data iliyokusanywa kutoka kwa zaidi ya watu 1,600.
Wengi wao walisema kuwa visa vya ghasia vimepungua.
Hata hivyo, wasiwasi mkubwa ungali kuhusu mashambulizi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Al Shabaab na wakazi kukosa imani na taasisi za usalama.
Somalia imekuwa ikikumbwa na ghasia kwa zaidi ya miongo miwili.
Licha ya hali hiyo maelfu ya wasomali waliokimbilia mataifa ya kigeni wamekuwa wakirejea nyumbani kujenga upya nchi yao kwani hali ya usalama angalau imeimarika katika miaka ya hivi karibuni.
Wapiganaji wa Al-Shabab, walifurushwa kutoka Mogadishu mwaka 2011 lakini mara kwa mara kundi hilo hufanya mashambulizi maeneo ya mjini na bado wanadhibiti maeneo mengi ya vijijini.
Mnamo mwezi Februari, wapiganaji wa kundi hilo, walishambulia jengo la Villa Somalia, ambalo lina makazi ya Rais na taasisi zengine za serikali na kuwaua watu 11.
Kulingana na utafiti huo, wakazi wengi walisema kuwa bado hawajashuhudia makabiliano ya kikabila katika mwaka mmoja uliopita.
Hata hivyo, watu wengi bado wanasema wana wasiwasi kuhusu mzozo kati ya jamii mbali mbali na mashambulizi yanayofanywa na Al Shabaab.
Pia walisema kuwa hawana imani na taasisi za usalama pamoja na idara ya mahakama.
Katika eneo moja, asilimia 66 ya wakazi waliohojiwa, walisema walionelea bora kuripoti utata wowote kwa viongozi wa kijamii huku asilimia 7 pekee wakitafuta msaada wa polisi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment