Timu ya Michezo ya Wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo ya haswa kuwa mfano katika mashindano ya SHIMIWI


Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali Watu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Titus Mkapa akimkaribisha Mwenyekiti wa timu ya Wizara HUM Sports Club (hayupo pichani) ili atoa salama za wachezaji kwa mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (HUM Sports Club) Dkt. Margareth Mtaki akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo inayotarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mshindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo inayotarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mshindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimkabidhi zawadi Mwanamichezo aliyeiletea Wizara ushindi katika mashindano ya SHIMIWI na Meimosi mwaka jana Bibi. Niuka Chande. Mchezaji huyo aliibuka mshindi katika michezo ya Draft na kurusha Tufe na kuiletea Wizara vikombe viwili. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Timu ya Wizara Dkt. Margareth Mtaki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Wizara hiyo wanatarajia kwenda mjini Morogoro kesho kwa ajili ya mashindano ya SHIMIWI yatakayoanza kuanzia tarehe 27 septemba hadi Oktoba 11.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akiwa amenyanyua juu Kikombe cha ushindi wa kwanza kwa mchezo wa Draft katika mashindano ya SHIMIWI mwaka jana ambacho kilinyakuliwa na mchezaji watimu ya Wizara ya Habari Bibi. Niuka Chande (mwenye taki suti nyeusi)kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel akifurahia
Baadhi ya wachezaji wa timu ya HUM Sports Club wakitoa salaam za timu yao kwa mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo wanakwenda mjini Morogoro kushiriki mashindano ya SHIMIWI yanayotarajiw kuanza tarehe 27 mwezi huu na kumalizika tarehe 11 Oktoba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu ya Wizara itakayoshiriki mashindano ya SHIMIWI mwaka huu.Waliokaa kutoa kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa TBC Joyceline Lugora, Mwakilishi wa Kampuni ya Water.Com(T) Ltd Juma Rajab Mboge, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Timu ya HUM Sports Club Dkt. Margareth Mtaki. Picha zote na Frank Shija, WHVUM.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment