Afisa
Uhamiaji wa Kasumulu mpakani mwa Tanzania na Malawi, Elihuruma Mndeme
akizungumzia hali halisi ya mpaka na maandalizi ya kukabiliana na
ugonjwa wa Ebola.
Barabara ya kuingilia Mpaka wa Kasumulu
Hapa ni eneo la Tanzania kabla haujaingia katika Geti la Uhamiaji
Afisa Afya wa Mpakani Kasumulu, Ryoba Maijo akielezea jinsi walivyojipanga kukabiliana na ugonjwa wa Ebola .
Waandishi wa Habari wakiendelea kuchukua Taarifa Katika ofisi za Uhamiaji Kasumulu
Shughuli mbalimbali zikiendelea upande unaounganisha Boda ya Tanzania na Malawi
Afisa Uhamiaji wa Kasumulu mpakani mwa Tanzania na Malawi, Elihuruma Mndeme akionesha mpaka wa Tanzania na Malawi
Hapa
ni katikati ya Mpaka wa Tanzania na Malawi , Hapa waandishi wa habari
wakiuliza Maswali na kupata taarifa zaidi ya mpaka huo na Mwenyeji wao Afisa Uhamiaji wa Kasumulu mpakani mwa Tanzania na Malawi, Elihuruma Mndeme
***********
WAKATI kukiwa na hofu ya kuingia kwa ugonjwa wa
Ebola nchi jirani ya Congo, Maafisa uhamiaji mipakani wamejipanga kuhakikisha
hakuna mgeni atakayeingia nchini akiwa na dalili za ugonjwa huo.
Hayo yalibainishwa jana na Afisa Uhamiaji wa
Kasumulu mpakani mwa Tanzania na Malawi, Elihuruma Mndeme, alipokuwa
akizungumza na Mbeya yetu kuhusu mikakati ya kudhibiti wageni wanaoingia nchini
kutokuleta ugonjwa huo.
Mndemi alisema yeye pamoja na maafisa wake
wamejipanga kuhakikisha kila mgeni anayeingia nchini anakaguliwa vizuri kabla
ya kuruhusiwa kuendelea na safari kwa kuangalia kama ana dalili zozote za
Ebola.
Alisema ingawa bado hawajapelekewa vifaa maalumu
vya kupimia wageni wanaoingia nchini ili kuwabaini kama wanazo dalili za ugonjwa
huo lakini wanatumia mbinu mbali mbali kulingana na uzoefu walionao maafisa
ikiwemo kumwangalia mtu na kumhoji.
Aliongeza kuwa hivi sasa Afisa anayegongesha
stempu ni lazima ajiridhishe na maswali anayomuuliza mtu na sio kukimbilia
kukagua hati yake pasipo kuangalia alikotoka na anakokwenda kama ndiko kuliko
athirika na ugonjwa huo.
Alisema Mpaka wa
Kasumulu unachangamoto nyingi na kubwa ni kuwepo kwa njia za panya
nyingi jambo linalowawia vigumu maafisa kudhibiti uingiaji holela wa wageni
ambapo alisema kuna mipenyo 30 ya kuingilia nchini kutoka Nchi jirani ya
Malawi.
Kwa upande wake Afisa Afya wa Mpakani Kasumulu,
Ryoba Maijo,alisema idara yake
imejipanga kutokana na kuwepo kwa fomu maalumu ambayo mtu yeyote anayepita hapo
atakuwa akijaza taarifa zake ambazo zitambaini kama ana maambukizi au hana.
Alisema tangu ugonjwa huo kuripotiwa baadhi ya
Nchi idara hiyo imekuwa ikichukua tahadhari kubwa ili usije ukaingia nchini
kupitia mipakani hivyo kuwa makini na kila mgeni anayepita hapo.
Na Mbeya yetu
Na Mbeya yetu
0 maoni:
Post a Comment