UKRAINE:JESHI LAZIDIWA NGUVU NA WAASI

Jeshi la Ukraine linaendelea kupoteza baadhi ya maeneo na kuchukuliwa na waasi baada ya jeshi hilo kuanzisha hivi karibuni mashambulizi zidi ya waasi kwa lengo ya kuyaweka kwenye himaya yake maeneo yanayo shikiriwa 

waasi wanaendelea kuyateka baadhi ya maeneo ukiwemo uwanja wa ndege wa Lougansk ambao kwa sasa ni ngome yao tayari maafisa wa ngazi za juu jeshini wameanza kunyooshewa kidole .

kujiondoa kwa wanajeshi katika uwanja wa ndege wa Lougansk ni moja ya ishara ya kushindwa kwa jeshi kumudu mapigano yanayo endeshwa na waasi.kwa mujibu wa volodymyr Rouban ambaye ni afisa katika serikali ya Ukraine anaeshiriki mazungumzo ya kubadilishana wafungwa ,Takribani wanajeshi 700 wa Ukraine wameshikiliwa mateka hivi karibuni na waasi katika jimbo la Donetsk,Afisa huyo amebaini kwamba hali kwa sasa ni "tata"

wakati jeshi la Ukraine likijiandaa kuonyesha sura nzuri ya kuimalisha ulinzi dhidi ya waasi baadhi ya wanajeshi wamebaini kwamba wanakabiliwana ukosefu wa uwezo,hususani vifaa vya Jeshi Bataliani mmoja ya  wanajeshi imeamua kujiondoa katika uwanja wa mapigano hadi pale watakapo pata uwezo wa kushindana na waasi.

wanajeshi wasio na uzoefu katika vita wametumwa katika uwanja wa mapigano kama alivyo shuhudia mwanajeshi mmoja mwanamke 

Hata hivi baadhi ya maseneta wa marekani akiwemo rais wa halmashauri ya mambo ya nje kwenye Bunge la Marekani Robert Menendezo pamoja na baadhi ya wanasiasa wameomba jumatatu wiki hii kuitolea Ukraine msaada wa kijeshi hili iweze kupambana na waasi.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment