MOSHI:
JAIZMELALEO
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Jamal Malinzi amewataka makocha kujikita zaidi katika kuzalisha vipaji vya soka ili kuondoa uwepo wa nyota wengi wa kigeni wanaoingia kwa kasi nchini.
Akizungumza katika siku ya
mwisho ya mafunzo ya ukocha ngazi ya awali mkoani Kilimanjaro iliyoandaliwa na
Mkombozi Vocational Training Centre na kufanyika mjini Moshi alisema nyota
wengi wa kigeni wamekuwa wakitiririka nchini kwa kasi ya ajabu kusaka bahati
yao huku hazina ya wanasoka wa ndani ikiwa finyu.
Jamal alisema ni msimu wa nne
sasa katika Ligi kuu wafungaji bora wamekuwa ni nyota wa kigeni hali ambayo
imekuwa ikitengeneza timu ya taifa isiyo na kiwango cha juu.
Rais huyo aliongeza kusema
makocha waliohitimu mafunzo hayo wanapaswa kuitendea haki nafasi hiyo adhimu,
na kuwataka kuvitumia vyeti vyao sawasawa na maelekezo yake.
Hata hivyo Malinzi aliwataka
makocha kuepukana na usimba na uyanga katika kuvikuza vipaji vya soka kwani
siasa imetawala katika vilabu hivyo vikubwa hapa nchini, badala ya kuibua
vipaji imekuwa ikiua.
Aidha Jamal alisema mwaka ujao
TFF itatoa kozi ya kati (intermediate course) ya ukocha mkoani humo na kuongeza
kwamba Chuo cha Mkombozi kitaingizwa katika program ya vyuo 53 nchini ya kukuza
soka la wanawake chini ya hisani ya serikali ya Sweden.
Kozi hiyo ya majuma mawili
iliwakusanya makocha wa mchezo wa soka kutoka mkoani humo na kuratibiwa na chuo
hicho ambapo Malinzi aliongozana na Mwenyekiti wa vyama vya soka nchini Eliud
Mvela.
Katika ziara yake mkoani humo alikabidhiwa ekari 20 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa katika wilaya ya Siha.
0 maoni:
Post a Comment