Katika
dunia hii ya utandawazi, ushindani ni kitu kisichoepukika. Haijarishi
wewe unafanya biashara ya kuuza peni au una blogu yako au hata unauza
dhahabu. Utandawazi umeweza kuwafanya wanunuzi wawe na sauti na machaguo
mengi toka kila pande, pande hizi zinaweza kuwa hata nje ya mipaka ya
nchi. Pia, wanunuzi wamepewa uwanja mkubwa wa kuijadili na kupata
taarifa za biashara yako kwa urahisi zaidi, mitandao jamii ni moja ya
kitendea kazi kwenye hili.
Ingawa
ushindani ni mkubwa sanasana, lakini leo hii, kama utatembelea kwenye
biashara kadhaa nchini Tanzania, utakubaliana na mimi kuwa, wengi
tunafanya biashara kwa mazoea (business as usual)na ubunifu umekuwa
mdogo sana kwa makampuni mengi sana. Iwe ya serikali au hata ya watu
binafsi, iwe madogo yaliyoanza jana au hata yale yenye umri wa miongo.
Leo
hii ni kitu cha kawaida sana kwenda kwenye kibanda cha pesa na muhusika
akaanza kukuhudumia hata bila ya kukusalimia, kwa wenyewe wanasema,
"kama hakijaharibika, basi usikirekebishe (If it ain't broke, don't fix
it)", Na wengi tumekuwa tukiaminni hivyo, kama wateja wanakuja, basi
hakuna haja ya kuboresha. Sisi Dudumizi tunasema, maboresho ni wimbo wetu wa kila siku, hata hii blog ni zao la maboresho na marejesho.
Ukweli
ni kuwa, kwa wewe mtoa huduma za kipesa kutowachangamkia wateja, basi
wao wataamua kutafuta ATM ambapo siku hizi wanatoa huduma zote. Mfano
mzuri ulionitokea binafsi, wiki iliyopita nilienda Bank XX kwa ajili ya
kukata bima ya gari, nilipokelewa bila hata salamu, tena baada ya kung'a
macho sana bila kujua pakuanzia. Kitendo kile, kikanikera na nikaamua
kuondoka, nikaambiwa, kwa Tanzania, nenda AON, hawa wanajua wanachokifanya, nilipokelewa na kama mfalme, na nikamalizana nao ndani ya mudamchache sana.
Hii
inamaanisha, Benki XX ambayo ni ya wazawa, inapoteza wateja wengi sana
kwa kutojua nini wateja tunataka, kesho watakuj kulalamika atuwapi
nafasi wazawa.
Hiyo
ni mifano michache ambayo inaweza kukukimbizia wateja. Sasa, swali dogo
tu, je wahusika wanajua kinachoendelea? Jibu linaweza kuwa ndiyo au
hapana, ndiyo ni kuwa wanajua ila hawajui kama linawagharimu, na siyo ni
kuwa hawajui kama kuna njia za kuboresha. Hivyo leo tuangalie njia
chache unazoweza kutumika kuboresha ubora wa huduma yako.
Vizio vya Vipimo (Metrics)
Kuna
usemi unaosema, usipopima, basi hautoweza kuboresha, na unachopima ni
muenendo wa utendaji wa huduma. Kwakuwa lengo ni kuboresha, biashara
inaweza boreshwa kwenye huduma yenyewe, kwenye mfanyiko au kwenye
teknolojia inayoiendesha. Vizio vya vipimo vinavyoweza kuchukuliwa ni,
1. Vizio vya huduma (Service Metrics) 2. Vizio vya mfanyiko (Process
Metrics) na mwisho ni 3. Vizio vya Teknoloji (Technoloji Metrics), hebu
tuangalie moja baada ya nyingine.
1. Vizio vya Huduma (Service Metrics)
Vizio
vya huduma, hupima utendaji wa huduma husika, hii huangalia vitu kama
kuridhika kwa wateja (Overall customer satisfaction with a specific
service), gharama halisi za huduma na muda unaotumiwa kukamilisha huduma
husika (mfano ni kwenye mabenki nk).
Kwakuwa
lengo ni kumuhudumia mteja, sehemu hii itakupa picha ya kujua jinsi
gani huduma inavyofanya sokoni na mapokeleo yake toka kwa wateja. Hii
itakupa picha nzuri kwenye kupanga ukuaji, maboresho na hata ujio mpya.
Kumbuka, bila mteja, hakuna umuhimu wa huduma hata kama itatolewa bure.
2. Vizio vya mfanyiko (Process Metrics)
Vizio
hivi hukuwezesha kujua utendaji kazi / muingiliano kati ya idara au / na
wahusika. Ni vizio vya mfanyiko vitakavyokuwezesha kujua ni jinsi gani
watu wa marketing wanashindwa kufanya kazi zao kwa kuwa Meneja wao hana
uwezo wa kupitisha matumizi ya fedha bila kupata kibali toka kwa
Mkurugenzi mtendaji hata kama ni shilingi elfu moja.
Vizio
hivi ni kama vile, mara ngapi wateja wameshindwa kutuma hela toka kwenye
biashara yako kwakuwa haukuwa na salio, au ni wateja wangapi
wametatuliwa tatizo lao papo kwa hapo baada ya kupiga simu kwa wahudumu
wa wateja (binafsi ni mhanga wa hili kwa upande wa simu kwani mara zote,
sijawahi kutatuliwa tatizo langu kabla ya kuhamishwa idara zaidi ya
moja na mwishowe kuambiwa litatatuliwa ndani ya masaa 24).
Hivyo,
kwa kutumia vizio vya mfanyiko, utaweza kufahamu jinsi gani kazi
zinafanyika ndani ya biashara yako.Na jinsi gani utaweza kuziboresha ili
kuongeza ufanisi / ubora wa biashara yako.
3. Vizio vya Teknolojia (Technology Metrics)
Dunia
ya leo, tumegubikwa na rundo la Teknolojia, na sisi huwa tunasema," IT
si kitu (IT Doesnt Matter)",ikimaanisha, IT siyo kitu kama haitoweza
kuleta uthamani wa huduma (Service value). Kwa kuchukua vizio hivi,
utaweza kufahamu halisi ya miundo mbinu ya Teknolojia, jinsi Teknolojia
inatumika / ingetumika na inakunufaishaje.
Hapa
unaweza kuchukua vizio kama, ni idadi gani ya watembeleaji wa blogu yako
wanatumia simu za mkononi,matangazo ya kwenye mitandao,matumizi ya
barua pepe kwa mambo ya kampuni na yale yasiyo ya kikampuni, wateja
waliokuja tokea kwenye mitandao jamii nk.
Ni vipimo hivyo vinavyo hitajika kwenye kuboresha ubora wa huduma, vizio vinatakiwa vijulikane na vitumike. Pia, inashauriwa uvitumie kwa pamoja ili kupata matokeo bora. Kumbuka, hata kama hakijaharibisha, lazima ukiboreshe ili kisije kuharibika wakati unakihitaji kukitumia au kikafa kabisa.Ushindani ni mkubwa sanasana, ila ni ubora wa huduma yako ndioutakaokufanya uendelee kuwa sokoni.Endelea kuboresha mpaka siku ya mwisho.
0 maoni:
Post a Comment