Waarabu kuisaidia Marekani dhidi ya IS

Nchi 10 za kiarabu zimekubaliana kuisaidia Marekani kupambana na Islamic State.Taarifa hii inafuatia mkutano wa viongozi wa nchi hizo ikiwemo Saudi Arabia na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry mjini Jeddah.
Nchi hizo pia zimekubaliana kusimamisha misaada ya kifedha na nguvu kazi ya wapiganaji kwa kundi la Islamic State ambalo linashikilia maeneo makubwa katika nchi za Syria na Iraq.
Hata hivyo Bwana Kerry ametoa changamoto kwa nchi hizo za kiarabu kuwa zinapaswa kusaini makubaliano ya muungano wa kimataifa dhidi Islamic State kwa sababu wamekwisha tambua hatari mbele yao.
Mkutano baina ya Waziri huyo na viongozi wa eneo hilo la mashariki ya kati umekuja siku moja tu baada ya tangazo la Rais Barack Obama la mpango wa kujenga mshikamano dhidi ya kundi la Islamic State kwenye nchi za Syria na Iraq.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment