WATU watano wamehukumiwa kifungo cha
miaka 37 jela na kuchapwa viboko 24 kila mmoja baada ya kupatikana na
hatia ya kuvamia na kupora fedha benki ya NMB tawi la Maswa kwa kutumia
silaha.
Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga na kusikilizwa na Hakimu Mkazi wa
Mahakama hiyo, Neema Gasabile ambapo alitoa hukumu hiyo.
Aliwahukumu kifungo cha miaka 37 na
viboko 24 kila mmoja viboko 12 wakati wa kuingia na 12 wakati wa kutoka
baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka
kuwa kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume cha sheria.
Washitakiwa hao ni Kapama Hamis Ramadhan
(37), Mussa Athuman Buberwa (38), Amos Mathayo, Lucas Vincent Mabela
(40) na Zainabu Mchau (60) wote kwa pamoja walipatikana na hatia ya
makosa tisa ya jinai.
Mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo,
Mwendesha Mashitaka Mwanasheria wa Serikali Edith Tuka aliieleza
mahakama hiyo kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo
majira ya saa 6:00 mchana Julai 5, mwaka 2010 mjini Maswa.
0 maoni:
Post a Comment