Madiwani wa CUF wilayani Tanga,
wamesababisha kuahirishwa kwa muda wa zaidi ya saa tatu kikao cha kamati ya
fedha na uchumi wakipinga mjumbe mwengine, Mohamed Mambea, kushiriki kikao
hicho kwa madai si mjumbe halali.
Diwani huyo alikihama chama
hicho hivi karibuni na kujiunga na CCM.
Hali hiyo ilimlazimu Mstahiki
Meya wa jiji la Tanga, Omari Guled, kuahirisha kwa muda kikoa hicho ili kutoa
fursa ya kusikiliza hoja zao.
Kikao hicho cha kamati kilikuwa
kinajadili hoja zilizotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa
ajili ya kuwasilisha kwenye kikoa cha Mkuu wa Mkoa, Chiku Gallawa hivi
karibuni.
Akizungumza na gazeti hilo,
Naibu Meya Muzamil Shemdoe, alisema kitendo kilichofanywa na Madiwani WA CUF ni
uhuni na ni tukio la kusikitisha kwani badala ya kufuata taratibu wao walivamia
mkutano.
“Hawa wamefanya uhuni, sheria
ipo na taratibu zipo za kufuata ili sherai iweze kufanya kazi ipasavyo sasa wao
badala ya kufuata utaratibu wa kimaandishi wao wanakurupuka na kuja kutuharibia
kikao chetu,” alisema.
Alisema kikao kilianza majira
ya saa nne asubuhi na baada ya kama nusu saa ndipo wadiwani hao kama saba
walipovamia kikoa hicho na kumtaka Mambea atokee kwenye kamati hiyo kwani sio
mjumbe halali na hana haki ya kushiriki.
Hata hivyo madiwani hao wakiongozwa na Diwani wa kata ya Ngamiani Kusini, Mussa Mbaruku, walilazimika kwenda ofisi za Mkurungenzi wa jiji, Juliana Malange, kuelekezwa taratibu za kufuata.
0 maoni:
Post a Comment