Watu 200 wauawa na mafuriko huko Kashmir


Mafuriko katika eneo la Kashmir
Mafuriko yamewaua zaidi ya watu 200 nchini India na Pakistan huku watabiri wa hali ya hewa wakisema kuwa mvua zaidi inatarajiwa kunyesha.
Majeshi ya mataifa yote mawili yanaongoza shughuli za uokoaji kwa kutumia ndege ili kujaribu kuyafikia maeneo ya vijijini.
Takriban watu 100 wamefariki katika eneo la kashmir linalosimamiwa na India baada ya mafuriko hayo kuyasomba makaazi mbali na kusababisha maporomoko.
Maafisa katika eneo la kashmir linalosimamiwa na Pakistan wamesema kuwa takriban watu 110 waliuawa.
Ni mafuriko mabaya kutokea katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka sitini baada ya kuwashangaza raia waliodhani kwamba msimu wa kila mwaka wa upepo mkali ulikuwa umekwisha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment