Balozi Seif Atembelea Ujenzi wa Daraja la Kisasa Kigamboni Dar.

Na Othman Khamis. OMPR.


Mradi mkubwa wa ujenzi wa Daraja la Kisasa linalojengwa katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es salaam unatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi Mwezi Julai mwaka ujao wa 2015 baada ya kukamilika ujenzi wake mwezi wa June mwaka ujao.



Meneja mradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Tanzania { NSSF } Mhandisi Karim Mattaka alieleza hayo wakati wa ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofanya ziara maalum kukagua ujenzi wa Miradi mikubwa inayogharamiwa na mfuko huo.



Miradi hiyo muhimu kwa ustawi wa jamii ni pamoja na  Daraja hilo  la Kigamboni na Nyumba za Mkopo Nafuu zinazojengwa katika eneo la Kijichi Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam.



Mhandisi Mattaka alisema miradi hiyo inayokwenda sambamba ujenzi wake itakapokamilika itasaidia kupunguza msongamano wa wasafiri wa maeneo hayo pamoja na makaazi hasa vijana wanaoanza ajira mpya katika taasisi mbali mbali za umma.



Meneja Mradi huyo wa NSSF alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ujenzi huo uliofikia hatua ya zaidi ya asilimia 60% unafanywa na Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi wa Madaraja kutoka Jamuhuri ya Watu wa China { China Mager Bridges }.



Alifahamisha kwamba Daraja hilo lenye urefu wa nusu Kilomita litakuwa na bara bara mbili zenye uwezo wa kupitisha magari matatu  kwenye njia tatu kwa wakati mmoja kwa kila bara bara.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment