Harakati
za kutafuta tiketi ya kufuzu kuelekea nchini Ufaransa mwaka 2016 kwenye
michuano ya soka ya mataifa bara la Ulaya ziliendelea tena usiku wa
kuamkia leo wakati timu kadhaa ziliposhuka dimbani.
Mabingwa
watetezi Hispania walikuwa wageni dhidi ya Luxembourg , hadi mwisho wa
mchezo huo wageni Hispania wakafanikiwa kuibuka washindi baada ya
kuwaadhibu wenyeji wao kwa jumla ya mabao 4-o. Russia ilishindwa
kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kugawana point
na wageni wao Moldova kwa kutoka sare ya bao 1-1.Kwingineko England iliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Estonia.Nayo Swedeni nako kulikuwa na hekaheka zilizowakutanisha wenyeji Sweden dhidi ya Liechtenstein.
Hadi mwisho wa mchezo huo wenyeji wakafanikiwa kuwagaragaza wapinzani wao kwa jumla ya mabao 2 kwa mshangao.Austria ikaisambaratisha Montenegro kwa jumla ya goli 1 kwa bila, wakati Slovenia walipowavunjia heshima wenyeji wao Lithuania kwa kuwasasambua bila huruma kwa mabao 2-0 huku Belarus ikitafuta majibu ya kuwapa mashabiki wake baada ya kudondokea pua kwakufungwa mabao 3-1 dhidi ya Slovakia.
0 maoni:
Post a Comment