India yapiga hatua katika kuwapatia visaidizi walemavu


 Waandishi wa habari kutoka nchi mbali mbali wakiangalia viungo bandia vya binadamu, walipotembelea kituo kikuu kinachotengeneza viungo hivyo nchini India.
Waandishi wa habari kutoka nchi mbali mbali wakiangalia viungo bandia vya binadamu, walipotembelea kituo kikuu kinachotengeneza viungo hivyo nchini India.
Na: Hassan Hamad-India.

Kiasi cha wagonjwa 65,000 wenye ulemavu wa aina tofauti wanapatiwa visaidizi pamoja na matibabu kila mwaka nchini India, hatua ambayo huwawezesha kuendelea na shughuli zao za kimaisha kama kawaida.

Meneja wa kituo kikuu cha viungo bandia vya binadamu katika mji wa Jaipur jimbo la Rajasthan kaskazini mwa India, Om Prakash Sharma ameeleza hayo mbele ya waandishi wa habari kutoka baadhi ya nchi za Afrika, Asia na Latin America waliofika kituoni hapo hivi karibuni kwa ziara maalum ya kimasomo.

Sharma amesema kituo hicho kijulikanacho kwa jina la “Bhagwan Mahaveer Viklang Sahayata Samiti (BMVSS), ndio kituo kikubwa zaidi duniani kinachojihusisha na utengenezaji na utoaji wa viungo bandia vya binadamu vikiwemo miguu na mikono.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment