Ujuzi wa sayansi wa kibinadamu umeongezeka mara mbili kwa kipindi cha miaka mitano tu ya mwanzo wa karne ya ishirini na moja. mwaka wa 1300 katika maktaba ya chuo kikuu cha Sorbonne,Paris,Ufaransa,kulikuwa na vitabu 1338 tu,lakini sasa maktaba ya marekani iitwayo Library of Congress iliyokuwa mjini Washington,D.C,ni maktaba iliyokubwa zaidi katika nchi hiyo,yenye vitabu na magazeti milioni 98 siku hizi mtu awezi kupitia mtandao wa Inteneti kufikisha ujuzi huo katika pembe nyingine ya ulimwengu.
kwa kweli ujuzi katika uwanja wa elimu umekuwa na mwendo wa kasi.Si zaidi ya miaka 130 tangu Dk. Theodor Billroth alipo faulu kwa mara ya kwanza kufanya upasuaji wa tumbo ukilinganisha na siku hizi ujuzi wa kiganga umefikia hatua kubwa.
kabla ya miaka 180 mwana Fizikia wa kingereza Yohana Dalton alijishughulisha sana na kuipanga dhana yake ya elimu ya atomi.Siku hizi viini vyenyewe nishati ya atomi hupasuka na kufanya kazi ya kutoa nguvu ya kuifanya dunia yetu kuwa paradiso na kwa upande mwingine kuifanya kuwa mzoga.
katika mwaka wa 1780 ndugu W.Herscel kwa darubini aliyo itengeneza mwenyewe aligundua sayari iitwayo Uranus. iko umbali wa kilometa milioni 2,870 kutoka katika jua, kiasi ambacho aiwezi kuonekana kwa gharama nafuu ya macho ya mwili.
Fikiria maendeleo ya tekinolojia na uvumbuzi ulio fanywa katika karne mbili zilizo pita Gari la moshi(mwaka 1825),motokaa(1885),ndege ulaya(1903),eropleni aina ya jet ya (1931),simu ya mdomo telephone 1876 na Redio (1895),televisheni na kompyuta za mahesabu (1930)
Na satellite hiyo ambayo huizunguka dunia yetu kilometa 590 kwenda juu inayo darubuni ya kuweza kuchukuwa picha duniani hata ya panya mdogo anaye tambaa umbali wa kilometa 700! moja wapo ya darubini kubwa ya kioo chenye kipenyo cha mita 5 iliyoko katika mlima Palomar,inauwezo wa kukumba mwanga mwingi sawa na macho ya binadamu
sasa kwa kutumia satelite bora zaidi aina ya KH-12 mwanadamu anaweza kuiangalia dunia vizuri zaidi kama vile mtu anaye fichua juu ya Dunia herufi ya ukubwa wa mita moja ya mtu,zaidi ya hayo kwa kutumia satelite Elintt izungukayo kilometa 36,000 juu aweza kuisikia redio ya mkononi Duniani
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 maoni:
Post a Comment