Rais wa zamani wa Madagascar akamatwa


Marc Ravalomanana alikimbia uhamishoni baada ya kuondolew amamlakani
Aliyekuwa rais wa Madagascar Marc Ravalomanana amekamatwa muda mfupi baada ya yeye kurejea nyumbani baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka mitano
Mwandhi wa bbc mjini Antananarivo amesema kuwa vitoa machozi vilirushwa na badaye vikosi vya usalama vikaonekana nje ya nyumba yake.
Serikali ya kisiwa hicho cha bahari Hindi mara nyingi imezuia kurudi kwake nyumbani tangu mpinzani wake Andry Rajoeline amuondoe madarakani kwa njia ya kijeshi.
Miaka minne iliyopita rais huyo wa zamani alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani bila ya yeye kuwepo mahakani kutokana na mauaji ya watu 30 wafuasi wa upinzani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment