Kinana aahidi wakulima

Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameahidi kulitafutia ufumbuzi tatizo la wakulima wa chai katika Jimbo la Bumbuli ndani ya mwezi mmoja ujao.  Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji.  Kinana aliwalaumu viongozi wa Serikali ya mkoa kutumia muda mrefu kushughulikia matatizo ya wakulima na kutolea mfano tatizo la kiwanda hicho lililoanza mwaka 2008.  “Mgogoro huu ni wa siku nyingi, watu wanatupiana mpira tu...Badala ya kuchukua hatua kuutatua, wao wanaleta porojo. Viongozi wa Serikali wanawapuuza wakulima wakati wao mambo yao yako safi,” alisema.  Kinana aliwaambia wananchi hao kuwa atalifikisha suala hilo katika Kamati Kuu ya CCM inayohudhuriwa na viongozi wote wa juu nchini.  “Tutakwenda kujifungia na kuulizana maswali magumu... ni lazima walioshindwa kulishughulikia suala hili wawajibike, kama hawataki kuwajibika kwa hiari basi wawajibishwe,” alisema.  Alibainisha kuwa kumekuwa na kulindana ndani ya Serikali na ndio maana viongozi wanaoshindwa kushughulikia matatizo ya wananchi wanaendelea na utumishi bila ya kuchukuliwa hatua zozote kwa haraka.  Awali, wananchi waliohudhuria mkutano huo walimtimua diwani wao, Richard Mbuguni ambaye walimtuhumu kushirikiana na mwekezaji huyo kuwadhulumu wakulima. Wananchi hao walifanya hivyo baada ya mwenyekiti wa wakulima wadogo wa chai katika eneo hilo, Almas Shamshama kumtaka kiongozi huyo kuondoka katika mkutano huo.Kinana aahidi kusaidia wakulima Mponde SHARE BOOKMARKPRINTEMAILRATING     Na Rais Said, Mwananchi  Posted  Jumatano,Oktoba1  2014  saa 8:14 AM KWA UFUPI  Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji. SHARE THIS STORY        0  inShare   Bumbuli. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameahidi kulitafutia ufumbuzi tatizo la wakulima wa chai katika Jimbo la Bumbuli ndani ya mwezi mmoja ujao.  Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji.  Kinana aliwalaumu viongozi wa Serikali ya mkoa kutumia muda mrefu kushughulikia matatizo ya wakulima na kutolea mfano tatizo la kiwanda hicho lililoanza mwaka 2008.  “Mgogoro huu ni wa siku nyingi, watu wanatupiana mpira tu...Badala ya kuchukua hatua kuutatua, wao wanaleta porojo. Viongozi wa Serikali wanawapuuza wakulima wakati wao mambo yao yako safi,” alisema.  Kinana aliwaambia wananchi hao kuwa atalifikisha suala hilo katika Kamati Kuu ya CCM inayohudhuriwa na viongozi wote wa juu nchini.  “Tutakwenda kujifungia na kuulizana maswali magumu... ni lazima walioshindwa kulishughulikia suala hili wawajibike, kama hawataki kuwajibika kwa hiari basi wawajibishwe,” alisema.  Alibainisha kuwa kumekuwa na kulindana ndani ya Serikali na ndio maana viongozi wanaoshindwa kushughulikia matatizo ya wananchi wanaendelea na utumishi bila ya kuchukuliwa hatua zozote kwa haraka.  Awali, wananchi waliohudhuria mkutano huo walimtimua diwani wao, Richard Mbuguni ambaye walimtuhumu kushirikiana na mwekezaji huyo kuwadhulumu wakulima. Wananchi hao walifanya hivyo baada ya mwenyekiti wa wakulima wadogo wa chai katika eneo hilo, Almas Shamshama kumtaka kiongozi huyo kuondoka katika mkutano huo.
Na Mwananchi 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment