TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Miaka 29 iliyopita sawa na siku kama ya leo ya tarehe mosi Oktoba mwaka 1985 ndege za kijeshi za utawala haramu wa israel ziliyashambulia makao ya harakati za ukombozi wa palestina (PLO) huko Tunisia ,watu wapatao 70 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia mashambulio hayo.PLO ilikuwa imeamishia makao yao Tunisia kutoka Lebanon baada ya mashambulio ya kijeshi ya utawala haramu wa Israel nchini humo mwaka 1982.Hata hivyo ungwaji mkono wa Marekani kwa utawala huo ulilifanya baraza la usalama la umoja wa mataifa lishindwe kuchukua hatua zozote za maana dhidi ya tel Aviv 

Na siku kama ya leo miaka 54 iliyopita nchi ya Nigeria ilipata uhuru wareno waliwasili Nigeria katika karne ya 15 na mkoloni mwingereza naye akawasili katika nchi hiyo karne ya 16 katika karne ya 17 ardhi iligeuzwa na kuwa moja kati ya vivutio vikubwa na muhimu vya biashara ya utumwa .mwishoni mwa karne ya 19 vikosi vya jeshi la uingereza vilidhibiti kikamilifu ardhi ya Nigeria,mwaka 1914 Uingereza ilifanikiwa kuziunganisha nchi mbili za nigeria ya kaskazini na kusini zilizokuwa chini ya udhibiti wa kuunda koloni moja la Nigeria.Miaka 10 baadaye nchi hiyo ilijitangazia utawala ndani yake hatimaye baada ya kupita misukosuko kama hii mengi.Nigeria ilipata Uhuru siku kama ya leo.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment