Vitambulisho vya NIDA vyasifiwa


Na Amina Omari, Tanga
UAMUZI wa serikali kuchagua teknolojia ya SMART CARD kutumika katika vitambulisho vinavyozalishwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) umeipa Tanzania sifa kubwa barani Afrika.

Hayo yalibainishwa na Mkurungezi wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari kutoka (NIDA), Joseph Makani, wakati akisoma hotuba kwa niaba ya  Mkurungenzi Mkuu, wakati wa uzinduzi wa zoezi la usajili na utambuzi wa watu mkoa wa Tanga.

Alisema hatua hiyo itasaidia taifa na watu wake kuleta mabadiliko makubwa katika nyanja za kiuchumi, kijamii kutokana na kuwepo kumbukumbu za taarifa sahihi kuhusu hali zao.

Aliwaomba watendaji kuhakikisha wanawajibika ipasavyo kuhakikisha zoezi la usajili na utambuzi kwa mkoa wa Tanga, linafanikiwa kwa ufanisi.


Nae Mkuu wa mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, aliwataka viongozi kuwapatia maelezo muhimu watendaji wa mitaa, vijiji na kata kuhusu namna bora ya ujazaji wa fomu za vitambulisho
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment