15 wakamatwa kwa mauaji Mombasa

 
 
Polisi wakifanya msako Mombasa
Polisi mjini Mombasa wamewakamata watu 15 kuhusiana na mauaji ya watu wanne usiku wa kuamkia leo mjini humo.
Lakini wamekanusha kuwa mauaji hayo yalihusishwa na msako wa polisi dhidi ya misikiti inayotoa mafunzo ya itikadi kali mjini humo.
Hali ya taharuki bado iko juu katika baadhi ya maeneo mjini humo huku polisi wakiendelea kushika doria mjini humo.
Kamishna mkuu wa Mombasa, Nelson Marwa anasema kuwa wale wote waliohusishwa na mauaji hayo ya watu wanne kwa kuwadunga visu, walikodiwa na mwanasiasa katika mtaa wa Kisauni.
Marwa hata hivyo amesema idadi ya wale waliouawa sio watu wanne bali ni watatu.
Hata hivyo jamaa wa waliouawa walithibitisha idadi yao kuwa watu wanne ambao walifariki baada ya kudungwa visu.
Wengine zaidi ya 12 walijeruhiwa kwenye tukio hilo ambalo limejhusishwa na vijana wenye itikadi kali za kidini.
Zaidi ya vijana 250 walikamatwa baada ya kupatikana na maguruneti pamoja na silaha nyinginezo kwenye msako uliofanywa Jumatatu asubuhi.
Viongozi wa kiisilamu na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu wamelaani msako huo ambao wanasema utarejesha tu hisia za waisilamu kulengwa na maafisa usalama.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment