Côte d'Ivoire: wanajeshi wanungunika




Wanajeshi wa Cote d'Ivoire wakizuia barabara zinazoingia katika eneo la kibiashara la Plateau, Abidjan, Novemba 18 mwaka 2014.

Wanajeshi wa Cote d'Ivoire wakizuia barabara zinazoingia katika eneo la kibiashara la Plateau, Abidjan, Novemba 18 mwaka 2014.

Na RFI
Wanajeshi wanaodai kupandishwa vyeo na kuongezwa mshahara nchini Cote d'Ivoire wameandamana Jumanne Novemba 18 katika mji mkuu wa Cote d'Ivoire, Abidjan na miji mingine muhimu, ukiwemo mji wa Bouaké.

Waziri wa Ulinzi Paul Koffi Koffi ametangaza kuchukua baadhi ya hatua.

Waziri wa Ulinzi paul Koffi Koffi ameahidi kuwa wanajeshi hao watapewa mishahara yao hivi karibuni.

" Nusu ya malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi wa zamani 476 wa FDS itatolewa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2014 na nusu nyingine itatolewa mwisho wa mwezi Desemba mwaka 2014", amesema Waziri wa Ulinzi Paul Koffi Koffi. Waziri huyo wa ulinzi amewataka wanajeshi kurejea kambini.

Katika mji wa Bouaké, wanajeshi wamedhibiti majengo ya shirika la utangazaji la RTI kwa muda wa saa moj ana nusu.

Kwa mujibu wa mmoja kati ya viongozi wa RTI, wanajeshi wanaomba maisha yao yaweze kuboreshwa, mazingira ya kazi na walipwe malimbikizo ya mishahara yao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment