Stori: Imelda Mtema
Staa wa
kiume wa sinema za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, kwa mara nyingine
alilazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar baada ya
kudaiwa kula chakula kinachosadikika kuwa na sumu (poisonous food).(P.T)
Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ akiwa hoi hospitalini.
Akizungumza
na mwandishi wetu wikiendi iliyopita Dk Cheni alisema kuwa alikuwa
mshehereshaji (MC) kwenye harusi moja iliyofanyika maeneo ya Sinza
jijini Dar ndipo akala chakula hicho ambapo muda mfupi baadaye alianza
kujisikia vibaya ‘kichina’.
Staa huyo
alisema kuwa baada ya hatua chache kutoka ukumbini, tumbo lilianza
kumuuma kisha akaishiwa nguvu ndipo akaweka gari pembeni na kupiga simu
kwa ndugu kuomba msaada.
Dk Cheni aliendelea kueleza kuwa baada ya kupata msaada moja kwa moja alipelekwa kwenye Hospitali ya Burhani jijini Dar.
Dk Cheni aliendelea kueleza kuwa baada ya kupata msaada moja kwa moja alipelekwa kwenye Hospitali ya Burhani jijini Dar.
‘Dk Cheni’,
Alisema
kuwa baadaye alihamishiwa kwenye Hospitali ya TMJ ambapo madaktari
walipompima waligundua alikuwa amekula chakula chenye sumu ndipo
wakampatia matibabu na kulazwa.
Alisema siku ya pili yake aliruhusiwa huku akisema kitendo hicho kimemsikitisha mno.
Alisema siku ya pili yake aliruhusiwa huku akisema kitendo hicho kimemsikitisha mno.
Siyo mara
ya kwanza kwa Dk Cheni kulishwa chakula chenye sumu kwani safari hii ni
mara ya pili ambapo mwaka jana alilazwa tena kwa ishu kama hiyo, jambo
ambalo haelewi kwa nini inakuwa hivyo
0 maoni:
Post a Comment