Mfichua
siri kuhusu tuhuma za rushwa kutolewa na Qatar ili kuiwezesha nchi hiyo
kushinda nafasi ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022
ameiambia BBC kuwa anaishi kwa hofu kutokana na hatua yake hiyo.
Mwaka
2011, Phaedra al-Majid alidai kuwa maafisa wa Qatar walijitolea
kuwalipa maafisa watatu wa vyama vya soka barani Afrika kiasi cha dola
milioni moja na nusu ili kuiunga mkono Qatar kuwa mwenyeji wa michuano
hiyo mikubwa duniani.Kamati ya Qatar ya uandaaji wa Fainali za Kombe la Dunia imesema ushahidi wa Phaedra al-Majid ulitiliwa mashaka na timu ya uchunguzi ya FIFA, na kwamba tuhuma zote zilichunguzwa na kutupiliwa mbali.
0 maoni:
Post a Comment