Gharama
za unene wa kupitiliza duniani ni karibu sawa na utumiaji wa bidhaa za
tumbaku ukiwemo uvutaji wa sigara au sawa na gharama za vita na kubwa
kuliko unywaji wa pombe au mabadiliko ya tabia nchi, unasema utafiti.
Taasisi
ya The McKinsey Global Institute imesema inagharimu pauni za Uingereza
trilioni £1.3, au asilimia 2.8% ya shughuli ya kiuchumi kwa mwaka -
inagharimu pauni za Uingereza bilioni £47.Watu wapatao bilioni 2.1 - kiasi cha asilimia 30% ya idadi ya watu duniani- wana uzito wa kupita kiasi au wana vitambi, watafiti hao wamesema.
Wamesema hatua ambazo ni wajibu wa mtu binafsi, zinatakiwa kutumiwa ili kutatua tatizo hili.
Gharama ya fedha kwa wenye vitambi inazidi kuongezeka- kwa huduma za afya na kwa upana zaidi katika uchumi. Kwa kusababisha maradhi, kitambi kina madhara katika utendaji wa kazi na kupotea kwa tija.
Watafiti wanasema kuwa sera zenye mwelekeo zinahitajika kufikiriwa.
Dr Alison Tedstone, mkuu wa masuala ya lishe katika Public Health England (PHE), amesema: "Ripoti hiyo ni mchango mzuri katika mjadala wa vitambi. PHE imesema ujumbe wa elimu pekee haisaidii kutatua tatizo la unene wa kupitiliza."
Dr Tedstone amesema unene wa kupita kiasi unataka hatua za kitaifa na serikali za mitaa, viwanda na jamii kwa ujumla, na hakuna jibu moja katika kukabiliana na hali hiyo".
0 maoni:
Post a Comment