Zaidi
ya nusu ya raia wa Liberia waliokuwa na ajira mara baada ya mlipuko wa
ugonjwa hatari wa Ebola hawana ajira tena kwa sasa,umebainisha utafiti
wa banki ya dunia.
Hivi karibuni ripoti ya wataalam wa uchumi wa benk ya dunia waliarifu kuwa ugonjwa wa Ebola ungetarajiwa kugharimu ukanda uliokumbwa na ugonjwa huo kiasi cha dola billion tatu hadi nne.
Ebola imeleta madhara kwa takribani watu elfu 14 Afrika Magharibi,huku watu Zaidi ya 5,000 wamekufa huku 2,800 wakiwa ni kutoka Liberia.
Ana Revenga, ni afisa mwandamizi wa benki ya dunia hata kwa wale wanaoishi katika maeneo ambayo hajaathiriwa na ugonjwa huo wa Ebola nchini Liberia bado wanakumbwa na madhara hayo.
Taairifa hiyo ya benki ya dunia inasema sekta ya kilimo Liberia imeathirika kwa asilimia 70 kutokana na utafiti uliofanyika
0 maoni:
Post a Comment