IGAD yaipa S-Sudan wiki mbili


Viongozi wa IGAD

Pande mbili zinazopigana Sudan Kusini zimepewa siku 15 zaidi kumaliza vita vya karibu mwaka, na kuhitimisha makubaliano ya kugawana madaraka.
Iwapo hazikufanya hivyo, basi pande hizo mbili zitawekewa vikwazo na mataifa mengine ya Afrika Mashariki.
Msemaji wa Jumuia ya nchi za Pembe ya Afrika, (IGAD) alieleza kuwa baada ya mazungumzo ya siku mbili mjini Addis Ababa, pande zinazopigana Sudan Kusini zimekubali kusitisha vita moja-kwa-moja.
Pande hizo zilionywa yatayofwata iwapo zitavunja makubaliano, kama alivotamka msemaji wa IGAD.
"Makubaliano ya kusitisha mapigano yakivunjwa na upande wowote ule, hatua zinazofuata zitachukuliwa na Jumuia ya IGAD:
Mali za pande hizo zitazuwiliwa.
Wanasiasa watapigwa marufuku kusafiri katika eneo la IGAD
Silaha na risasi zitazuwiliwa kupelekwa Sudan Kusini, pamoja na zana zote zinazoweza kutumiwa kwenye vita"
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment