Jumuia ya wafanyakazi wa Afrika
Kusini, COSATU, imekitoa katika jumuia chama cha wachimba migodi, NUMSA -
chama kikubwa kabisa na chenye malalamiko mengi ya kisiasa katika
jumuia hiyo.
COSATU imchukua hatua hiyo baada ya NUMSA kulalamika
dhidi ya Rais Jacob Zuma, na kukataa kuunga mkono chama tawala cha ANC
katika uchaguzi wa awali mwaka huu.NUMSA ilimshutumu Rais Zuma kwamba haungi mkono tena masilahi ya wafanyakazi na kusema kuwa itaanzisha vuguvugu jipya la kishosalisti.
Kiongozi wa NUMSA, Irvin Jim, alisema kuwa COSATU - ambayo zamani ikiwatikisa mabosi wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi - sasa imepooza.
0 maoni:
Post a Comment