NQ Vault App bora kabisa kwa ajili ya kuficha picha na video zako


Simu zimekuwa ni sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku. Kuongezeka kwa huduma za mitandao ya kijamii, kamera bora kwa ajili ya kuchukulia matukio na picha, viwango bora vya app za muziki na vitu vingine vingi vinaifanya simu yako kuwa kama kiungo mojawapo cha mwili. 


Kwa sasa makampuni makubwa ya utengenezaji wa simu yamekuwa yakishindana kutoa matoleo ya simu yenye uwezo mkubwa hasa ule wa kamera. Uwezo wa kamera umekuwa ni moja ya vitu vinavyoifanya simu kuonekana bora au la.

Hii yote ni kutokana na ukweli kwamba wengi wa watumiaji wa simu za kisasa, smartphones wanapendelea kushare picha na video fupi katika mitandao ya kijamii kama instagram, facebook, twitter au whatsapp. Vipi linapokuja suala la uhifadhi wa picha hizi, hasa zile tunazopenda kupiga tukiwa maeneo ya faragha au baadhi ya picha ambazo hatupendi wengine wazione?

Hapa ndipo unapokuja umuhimu wa kuwa na app bora ya ulinzi na usalama wa picha zetu. Kuna app nyingi playstore na iTune Store kwa ajili ya uhifadhi na utunzaji wa picha na video za siri. Nyingi ni nzuri lakini hazikidhi moja kwa moja mahitaji ya mtumiaji wa kawaida wa simu.

Hapa ndipo NQ Vault inapoingia, Vaulty ni app bora kabisa kwa watumiaji wa simu za android. Vault kutoka kwa NQ Vault ina uwezo mkibwa sana linapokuja suala la utunzaji wa data zako siri.

  • Baadhi ya Faida za NQ Vault ni:
  • Kuficha picha na video na kuzifanya zisionekane hata kwa kuchomeka simu kwenye kompyuta
  • Kuficha sms na missed calls za baadhi ya namba zilizochaguliwa. 
  • Kubackup picha na taarifa zako za siri mtandaoni kulingana na uhitaki wako
  • Uwezo wa kuficha icon ya app yenyewe
  • Uwezo wa kulock app muhimu

Kuna vitu vingi zaidi unaweza ikafaidika navyo kwa kutumia app hii.

from Blogger http://ift.tt/2kVC5U8
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment