Unafahamu kuwa unaweza kujitengenezea pesa kupitia blogu yako?

Ulishawahi kujiuliza iwapo itafika siku moja kwamba utakuwa unapata pesa kutokana na blogu uliyoifungua mtandaoni? Najua pengine wazo hilo halikuwepo awali wakati unaianzisha kwa sababu wengi wetu hufanya hivyo ili kujijengea wasifu mzuri hususani tuliomo kwenye tasnia ya uandishi wa habari.
Kila mtu anataka pesa na anatumia mbinu mbalimbali kuhakikisha anapata pesa. Jumia Travel ingependa kukufahamisha kuwa mbinu zifuatazo zinaweza kukufanikishia kujitengenezea pesa nzuri kupitia blogu yako. 
Kupitia matangazo ya CPC au CPM
CPC/PPC Ads (Cost per click or pay per click), ni matangazo ambayo huwekwa kwenye maudhui au pembezoni mwa blogu. Kila wakati ambapo msomaji hubonyeza tangazo hilo, wewe utakuwa ukilipwa kutokana na kitendo hiko.
Kwa upande mwingine, CPM Ads (cost per 1,000 impressions ads), ni aina ya matangazo ambayo hukulipa kiasi fulani cha pesa kutokana na kiasi gani cha watu waliolitembelea tangazo hilo kwenye mtandao wako.
Mitandao maarufu ambayo unaweza kujiunga na kufaidika na aina hiyo ya matangazo ni Google AdSense, Chitika, Infolinks na Media.net
Uza matangazo binafsi
Endapo utakuwa na wasomaji au watu wengi wanatembelea blogu yako basi wenye matangazo wenyewe watakufuata kukuomba uwawekee matangazo yao. Utofauti wa njia hii na ya hapo juu ni kwamba hakuna mtu wa kati au dalali, hii inamaanisha kwamba unaweza kuweka viwango vyako mwenyewe vya kutangaza. 
Itumie blogu yako kama njia ya kujitangaza kibiashara
Inawezekana pia ukaitumia blogu yako kama njia ya kuuza na kutangaza bidhaa zako mwenyewe. Hivyo basi badala ya kufikiria blogu yako itumike kukuingizia pesa pia unaweza kuitumia kama daraja kuwavuta wasomaji wako watembelee tovuti ya biashara yako.
Itumie blogu yako kujijengea jina na uaminifu
Kwa mfano, ukaanzisha blogu ambayo inahusu masuala ya benki pekee. Watu wataanza kusoma blogu yako na itaanza kupata umaarufu. Hatimaye utakuwa mtu mashuhuri na unayefahamika kwenye sekta ya benki. Hali hii inaweza kukupa fursa ya watu kukutaka ushiriki kwenye uandishi wa vitabu, kulipwa ili uzungumze kwenye midahalo au kuendesha semina kwa wafanyakazi. 
USHAURI WA KUZINGATIA: Kuanzisha blogu tu pekee yake sio sababu ya kukuingizia pesa, lazima uwekeze muda katika kuhakikisha inafanya vema. Hivyo basi, kabla ya kujikita katika uandishi wa blogu hakikisha unazingatia mambo yafuatayo:
Tengeneza maudhui yenye ubora
Blogu yako haitotengeneza pesa kama watu hawaisomi. Kwa sababu wao ndio watakaokuwa wanakuletea pesa kupitia kubonyeza matangazo au kununua bidhaa zako. Hivyo basi huna budi kuhakikisha unachokiandika kinawavutia watu kusoma.
Usipende kutumia muda mwingi kwenye blogu yako pekee
Safari ya kuwa na blogu yenye mafanikio makubwa inakwenda sambamba na kujijengea mahusiano mazuri na wadau mbalimbali. Wadau hao ni kama vile wadhamini, washirika wa kibiashara, pamoja na wanablogu wenzako ambao wanaweza kupendekeza wasomaji kuitembelea blogu yako. 
Usiogope kujaribu
Sio lazima njia hizo zote zilizotajwa hapo juu za kukuingizia kipato zitakufaa au kufanya kazi. Kwa hiyo usiogope kubadili mbinu kama haitofanya kazi kwako na kwa wasomaji wako. 
Kwa ujumla, mpaka blogu ianze kukuingizia kipato inahitaji bidii na jitihada za hali ya juu. Kwa hiyo Jumia Travel inakushauri wewe anza bila ya kuhofia kitu chochote kwani hatimaye itakuja kukulipa siku za usoni. Cha msingi ni kukumbuka kwamba sio lazima kuzitumia hizo njia zote zilizoorodhesha hapo juu, tazama wengine wanafanya nini kisha nawe anzia hapo.

from Blogger http://ift.tt/2laEDfu
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment