TOP 10: Angalia hapa orodha ya Laptop 10 kali zaidi sokoni kwa sasa

Soko la bidhaa za umeme (Electronic Gadgets) linabadilika kila kukicha huku makampuni tofauti yakijaribu kuonyeshana ubabe katika fani hii. Kuanzia na bidhaa kama simu, Kamera, TV, magari pamoja na kompyuta zote zimekuwa zikiboreshwa kila siku.
Wengi wamekuwa wakiuliza na kuomba ushauri juu ya mashine gani nzuri sokoni kwa sasa ili wanunue. Leo tumeamua kuwaletea orodha kamila ya Laptop 10 kali zinazobamba kwa sasa katika ulimwengu wa kiteknolojia. Orodha hii imepangwa kulingana na ubora wa mashine husika kwa kuangalia vitu kama Processor, Memory, Diski Hifadhi, Umbo na shape yake bila kusahau bei na maoni ya watumiaji.
1. Dell XPS 13 Ultra Book
Mashine hii kwa sasa ndio inaongoza katika soko kwa kuwa mashine kali zaidi kwa matumizi yote.
CPU: Intel Core i5 – i7 | Graphics: Intel HD Graphics 520 – Intel Iris Graphics 540 | RAM: 4GB – 8GB | Screen: 13.3-inch FH (1,920 x 1,080) – QHD+ (3,200 x 1,800) | Storage: 128GB – 256GB SSD
Faida
-Display nzuri ya kisasa
-Uzito mdogo, wembamba wa kutosha
Skylake processor
Bei nzuri
Hasara
Web Cam haipo kati
Batri linakufa kirahisi zaidi
2. Asus ZenBook UX305
Mashine kali zaidi ya MacBook kwa bei nafuu kutoka Asus. Ikiwa na viwango vyote vya kuitwa UltraBook. Faida kubwa ya mashine hii ni kukaa na chaji kwa muda mrefu zaidi.
CPU: Intel Core Intel Core M3-6Y30 – M7-6Y75 | Graphics: Intel HD Graphics 515 | RAM: 8GB | Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3200 x 1800) IPS display | Storage: 256GB – 512GB SSD
3. Razer Blade Stealth
Kwa wale jamaa zangu wapenda magemu hapa ndio mahala pao. Ikiwa imetengenezwa maalumu kwa ajili ya wapenzi wa magemu, mashine hii inakuja na keyboard inayoweza kubadilisha rangi ya kila key. Kuanzia vitufe vya A mpaka Z kila kimoja kinaweza kuwaka taa na rangi yake bila kusahau processor ya Kaby Lake Core i7 kutoka Intel.
CPU: Intel Core i7 | Graphics: Intel HD Graphics 620 | RAM: 8GB – 16GB | Screen: 12.5-inch, QHD+ (2,560 x 1,440) – 4K (3,840 x 2,160) IGZO LED-backlit multi-touch | Storage: 128GB – 1TB SSD
4. Samsung Notebook 9
Uzuri mkubwa wa mashine hii upo kwenye bei na huduma inazotoa. Bei yake ni nafuu sana ukilinganisha na uwezo wa mashine husika.
CPU: 2.3GHz Intel Core i5-6200U | Graphics: Intel HD Graphics 520 | RAM: 8GB | Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) LED anti-reflective display | Storage: 256GB
5. Surface Book
Ukiachana na ukali wa bei, mashine hii ilibidi ishike nafasi ya kwanza kwenye orodha hii kwa kuwa ndio mashine kali zaidi kutoka mwaka 2016 inayotumia Windows 10. Katika mshine hii Microsoft waliacha kazi wakafanya kazi katika kutengeneza umbo na kioo cha mashine hii. Pia uwezo wake wa kutumika kama tablet unaifanya mashine hii kuwa mpinzani wa kweli wa MacBook kama lengo la watengenezaji lilivyokuwa.
CPU: Intel Core i5 – i7 | Graphics: Intel HD graphics 520 – Nvidia GeForce graphics | RAM: 8GB – 16GB | Screen: 13.5-inch, 3,000 x 2,000 PixelSense Display | Storage: 128GB – 256GB PCIe3.0 SSD
6. HP Spectre
Hapa najua nimewafurahisha mashabiki wa HP, mashine hii ni ya pili kwa ubora kwa mwaka 2016 ukiacha HP Chromebook 13 ambayo ni ya bei nafuu zaidi kwa sababu ni Chrome Book (Mashine inayotumia mfumo endeshi wa Chromium kutoka Google). HP Spectre ni moto wa kuotea mbali linapokuja suala la kuhimili mikikimikiki ya kila siku.
CPU: Intel Core i5 – i7 | Graphics: Intel HD Graphics 520 | RAM: 8GB LPDDR3 SDRAM | Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) IPS UWVA WLED | Storage: 256GB – 512GB SSD
7. MacBook (2016)
Apple wametengeneza mashine hii wakiwa na lengo la kuwafurahisha mashabiki wake wanaopenda mashine zenye umbo zuri zaidi na zinazokaa na batri muda mrefu. Ikiwa na Processor ya Intel Skylake Core M mashine hii inakuja na teknolojia ya kisasa ya USB-C. Hauna sababu ya kuikosoa mashine hii kama wewe ni mtu unayekwenda na wakati.
CPU: Intel Core m3 – m5 | Graphics: Intel HD Graphics 515 | RAM: 8GB | Screen: 12-inch, 2304 x 1,440 LED-backlit IPS display | Storage: 256GB – 512GB SSD
8. Lenovo Yoga 900
Mashine hii kutoka kwa wakali Lenovo inakuja katika matoleo mawili, kama wewe ni mpenzi wa mashine nyembamba zaidi nakushauri ununue toleo la Lenovo Yoga 900S.
CPU: 2.5GHz Intel Core i7-6560U | Graphics: Intel Iris Graphics 540 | RAM: 8GB – 16GB | Screen: 13.3-inch QHD+ 3,200 x 1,800 IPS display | Storage: 512GB – 1TB SSD
9. MacBook Pro (15-inch, Late 2016)
Ukiachana na kipengere cha bei, mashine hii ilitakiwa ishike nafasi ya kwanza au ya pili ikichuana na Microsoft Surface Book. Kwa miaka mingi sasa MacBook Pro imekuwa chaguo la madesigner na madeveloper wengi. Hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa katika kufanikisha kazi nzito bila matatizo yoyote. Ikiwa na Retina Display mashine hii inavotia kila dakika kuiangalia.
CPU: Intel Core i7 | Graphics: AMD Radeon Pro 450 – 460 | RAM: 16GB | Screen: 15.4-inch Retina (2,880 x 1,800) LED-backlit IPS | Storage: 256GB – 2TB PCIe SSD
10. Lenovo ThinkPad X1 Yoga
Kwa miaka ya hivi karibuni Lenovo imekuwa ikitengeneza mashine za kuaminika katika soko. Ikiwa na processor ya Intel Core i5 na Core i 7 mashine imefunga orodha hii kwa ubora.
CPU: Intel Core i5 – i7 | Graphics: Intel HD Graphics 520 | RAM: 8GB | Screen: 14-inch, FHD (1,920 x 1,080) – WQHD (2560 x 1440) IPS touchscreen | Storage: 180GB – 512GB NVMe SSD
Toa maoni yako

from Blogger http://ift.tt/2lUIuwy
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment