Je wewe ni mtumiaji wa Laptop? Je laptop yako inapo onesha betri 100% unafanyaga nini? Je nifanyeje ili kufanya betri langu la laptop kuchukua muda mrefu zaidi likifanya kazi kwenye laptop yako?
Ni kweli kabisa imekuwa ikisumbua watu wengi sana kujua je ni salama kuendelea kuitumia laptop ikiwa kwenye chaji au La, Laptop ni kifaa kilicho tofauti kidogo na simu za mkononi kimuundo wa umeme, unashauriwa kuchomeka kwenye umeme kila mara unapo tumia laptop yako ili kulinda uhai wa betri.
Kwa kawaida kabisa laptop imeundwa kutumia umeme tu pale ilapochomekwa kwenye umeme hivyo betri lako litachajiwa na halitatumika mpaka chanzo cha umeme kinapo kosekana.
hivyo ni vizuri kutumia laptop ikiwa imechomekwa kwenye umeme muda wote ili kulinda uhai wa betri yako, hivyo siku ambayo hutakuwa na umeme utaweza tumia laptop yako kwa muda mrefu zaidi.
from Blogger http://ift.tt/2lUBGPi
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment